SERA YA FARAGHA
Selcom Pesa inatambua kuwa unajali faragha ya taarifa zako na jinsi ya matumizi na ushiriki wake. Taarifa hii inaeleza kwa kina sera yetu ya faragha. Tumejitolea kulinda taarifa zako binafsi na haki yako ya faragha. Tafadhali tumia muda mfupi kusoma na kuelewa taratibu zetu za faragha. Kwa kutumia programu ya duka.direct, unakubali taratibu zilizoelezwa kwenye Taarifa hii ya Faragha.
Ni Taarifa gani tunazokusanya?
Ili kujisajili, Selcom Pesa inahitaji ukamilishe usajili kwa kutumia namba yako halali ya simu, kitambulisho cha taifa (NIDA), na alama za kibayometriki. Taarifa zingine zinazokusanywa kutoka kwenye aplikesheni ni pamoja na majina, vitambulisho vya kuingia kwenye akaunti, na data za miamala.
Taarifa tunazokusanya zinatumikaje?
Tunaweza kutumia taarifa zako tunazozipata kupitia aplikesheni kwa madhumuni yafuatayo:
Kuboresha huduma zetu: Taarifa zako zinatuwezesha kukupa huduma bora zaidi.
Ubinafsishaji wa huduma: Taarifa zako zinatusaidia kukidhi mahitaji yako binafsi kama mteja
wetu wa thamani.
Kuboresha huduma kwa wateja: Taarifa zako zinatusaidia kujibu maombi yako ya huduma
kwa wateja na mahitaji ya usaidizi kwa ufanisi zaidi.
Kuboresha programu yetu: Taarifa zako na maoni yako yanatusaidia kuboresha programu yetu.
Kutuma barua pepe mara kwa mara: Anwani ya barua pepe na namba ya simu unazotoa
zinaweza kutumika kukutumia taarifa na masasisho kama vile taarifa za akaunti na taarifa
zingine zinazohusiana na akaunti yako.
Tunalindaje Taarifa Zako?
Tunajitahidi kulinda taarifa zako kupitia mfumo wa hatua za kiusalama za kiufundi. Tumetekeleza hatua zinazofaa za kiufundi na za shirika kulinda usalama wa taarifa zozote za kibinafsi tunazochakata.
Taarifa kuhusu wateja wetu ni sehemu muhimu ya biashara yetu, na hatupo katika biashara ya kuuza taarifa hizi kwa wahusika wengine. Hata hivyo, tunaweza kushiriki taarifa zako na wahusika wengine wanaotoa huduma kwa niaba yetu. Wahusika wetu wa tatu wote wanahitajika kuchukua hatua za kiusalama zinazofaa kulinda data zako kulingana na sera zetu. Hatutawaruhusu kutumia data zako kwa madhumuni yao binafsi. Tunawaruhusu kuchakata data zako kwa madhumuni maalum na kwa mujibu wa maagizo yetu.
Tunaweza pia kushiriki taarifa zako binafsi na wahusika wengine ikiwa tunalazimika kufichua au kushiriki taarifa zako binafsi ili kuzingatia wajibu wa kisheria au kulinda haki, mali, au usalama wa tovuti yetu, watumiaji wetu, na wengine. Ambapo data zako zinashirikiwa na wahusika wengine, tutahakikisha kushirikisha kiwango cha chini kinachohitajika.
Vipi Kuhusu Vidakuzi?
Hatutumii vidakuzi vyovyote.
Masasisho ya Sera ya Faragha
Sera yetu ya Faragha inasasishwa mara kwa mara, na masasisho yote yatatumwa kwenye ukurasa huu. Utajulishwa mara masasisho mapya yanapochapishwa.
Mawasiliano
Ikiwa una maswali yoyote kuhusu sera yetu ya faragha, unaweza kuwasiliana nasi kupitia barua pepe
help@selcompesa.app au piga simu bure 0800 714 888 / 0800 784 888.