JISOTI Suluhisho jipya la Mkopo wa haraka kupitia Selcom Pesa.

Katika harakati za kuendelea kuboresha huduma kwa wateja wetu, Selcom Pesa tumeleta huduma mpya ya mkopo kidijitali unakwenda kwa jina la JISOTI. Mkopo wa haraka, rahisi, na nafuu unaopatikana kupitia Selcom Pesa.

JISOTI ni nini?

JISOTI ni huduma ya mkopo wa kidijitali unaomuwezesha mtumiaji wa Selcom Pesa kupata mkopo kwa urahisi, hasa katika nyakati za dharura au anapohitaji msadaa wa haraka kwa ajili ya shughuli zao binafsi au biashara ndogo ndogo. Kupitia teknolojia ya kidijitali, mchakato wa kupata mkopo huu ni wa haraka.

Viwango vya Mkopo

Wateja wanaweza kuchagua kati ya mkopo wa siku 7 au 14, kulingana na uwezo wao wa kulipa. Kiasi cha mkopo kinapatikana kuanzia TZS 500 hadi TZS 500,000. Hivyo kuwapa uhuru wa kuchagua kiasi kinachokidhi mahitaji ya kifedha kwa wakati huo.

Ongeza Ustahiki wako

Ili kuongeza kiwango chako cha ustahiki wa mkopo, unaweza kutuma taarifa za miamala ya simu ya miezi mitatu ya hivi karibuni. Aplikesheni ya Selcom Pesa inakuongoza hatua kwa hatua namna ya kutuma taarifa hiyo kupitia (jisoti@selcompesa.app), hivyo kuhakikisha una nafasi ya kupata mkopo mkubwa zaidi kadri unavyoendelea kutumia huduma hii.

Faida za kutumia JISOTI

JISOTI ni suluhisho la haraka na la papo hapo wakati wa dharura hakuna foleni, hakuna makaratasi.

Historia ya mkopo, unapolipa kwa wakati, unajenga historia nzuri ya mikopo ambayo inaweza kukusaidia kupata mikopo mikubwa zaidi siku za usoni.

Upatikanaji rahisi, huduma inapatikana 24/7 kupitia simu yako popote ulipo.

Next
Next

Tumekuletea Mabando ya Miamala yanayokupa uhuru wa kifedha.