Kwa mara ya kwanza Tanzania, Selcom Pesa yazindua suluhisho jipya, nafuu la kifedha kupitia mabando ya miamala.

Kwa mara ya kwanza Tanzania, Selcom Pesa imeleta suluhisho jipya na nafuu zaidi kwa watumiaji wa huduma za kifedha nchini kupitia uzinduzi wa mabando ya miamala.

Mabando haya yametambulishwa kama 5 Kwa Jero, Wiki Boost, na Hello Mwezi.

Lengo kuu la huduma hii ya kimapinduzi ni kupunguza gharama za kufanya miamala ya kutuma pesa kwenda benki, mitandao ya simu pamoja na kufanya malipo kwenye Lipa Namba za mitandao ya simu na benki.

Taarifa muhimu za kila bando ni kama ifuatavyo;

1. 5 Kwa Jero – Bando la Siku

Hii ni kwa ajili ya watumiaji wanaohitaji kufanya miamala michache kwa haraka ndani ya siku. Ukijiunga na bando hili kwa TZS 500 tu utawezeshwa kufanya miamala 5 BURE ndani ya masaa 24 na kikomo cha kiwango ni TZS 1,000,000.

2. Wiki Boost – Bando la Wiki

Hili ni bando la kati linalofaa kwa wale wanaofanya miamala mingi ndani ya wiki. Ukijiunga na bando hili kwa TZS 2,500 tu utapata miamala 35 BURE ndani ya siku 7 na kikomo cha kiwango ni TZS 5,000,000.

3. Hello Mwezi – Bando la Mwezi

Kwa watumiaji wenye miamala mikubwa na wale wanaofanya Miamala mingi ndani ya mwezi. Ukijiunga kwa TZS 10,500 tu utawezeshwa kufanya miamala 150 BURE ndani ya siku 30. Kikomo cha kiwango cha bando hili ni TZS 50,000,000.

Kumbuka: endapo bando lako litaisha Unaweza kujiunga bando lingine. Pia Mabando haya ni kwa ajili ya miamala ya kutuma pesa kwenda benki, mitandao ya simu na kufanya malipo ya Lipa namba.

Kauli mbiu ya “Makato Madogo Kuliko” si maneno tu ni ahadi halisi ya Selcom Pesa kwa mamilioni ya Watanzania wanaofurahia huduma za kifedha zilizo nafuu na haraka.

Usichelewe, changamkia fursa hii ya kipekee ya kufanya miamala bila stress ya makato makubwa.

Ili kujiunga pakua aplikesheni ya Selcom Pesa kutoka Play Store Au App Store na kisha ujisajili mwenyewe ndani ya dakika chache ukitumia NIDA yako tu.

Next
Next

SELCOM YAZINDUA VITUO 10 VYA HUDUMA DAR ES SALAAM, KUWAFIKIA MAWAKALA NA WATEJA WA SELCOM PESA KWA UKARIBU ZAIDI