SELCOM YAZINDUA VITUO 10 VYA HUDUMA DAR ES SALAAM, KUWAFIKIA MAWAKALA NA WATEJA WA SELCOM PESA KWA UKARIBU ZAIDI
Dar es Salaam, 15 Mei 2025 – Selcom imezindua rasmi vituo vipya kumi vya Selcom Experience Centre jijini Dar es Salaam. Hatua hii inalenga kuboresha upatikanaji wa huduma kwa urahisi zaidi, ikiwemo utoaji wa float kwa mawakala pamoja na kuwezesha wateja wa Selcom Pesa kuongeza pesa kwenye akaunti zao kwa haraka, salama, na kwa makato madogo kuliko.
Kupitia vituo hivi vipya, mawakala wa Selcom sasa wanaweza kupata float kwa urahisi na haraka pia wateja wa Selcom Pesa wanaweza kufika katika vituo hivi kuongeza fedha kwenye akaunti zao papo hapo, kupata kadi yaani Selcom Pesa Mastercard, kupata msaada wa moja kwa moja kuhusu matumizi ya huduma mbalimbali zinazopatikana kwenye aplikesheni ya Selcom Pesa.
vituo hivi vimeboreshwa kuwa sehemu muhimu ya huduma kwa wateja wanaohitaji msaada wa moja kwa moja, elimu juu ya huduma, au wanaotaka kuwa sehemu ya mtandao wa Selcom kama mawakala. Usajili wa uwakala, upatikanaji wa POS mashine na roller, huduma za duka.direct na maelezo muhimu kuhusu Selcom.
Vituo vya Selcom Experience Centers vinapatikana katika maeneo ya Gongo la Mboto (Mtaa wa Banana), Manzese, Mbagala (Zakhem), Tabata Kinyerezi, Mbezi Mwisho Luis, Mbezi Tanki Bovu, Mwenge, Masaki, Kariakoo (Mtaa wa Uhuru na Nyamwezi), na Jamhuri Posta .Vituo hivi vimewekewa timu mahiri ya huduma kwa wateja na miundombinu inayowezesha utoaji wa huduma bora kwa wakati wote. Vituo vinafunguliwa kuanzia saa 2 Asubuhi mpaka saa 2 usiku, siku za Jumatatu mpaka Jumamosi, na saa 2 Asubuhi mpaka 11 jioni siku ya Jumapili.
Kwa kutumia aplikesheni ya Selcom Pesa, unaweza kufanya miamala kwa makato madogo kuliko ukilinganisha, mitandao mingine na benki okoa hadi 60% ukiwa na selcom pesa.Pakua sasa kupitia App Store au Play Store, na jisajili kwa kutumia namba yako ya NIDA pekee kwa dakika chache tu.Unatumia simu janja? Hakuna shida. Fanya miamala kirahisi kwa kupiga *150*35#.
Selcom Pesa Makato Madogo Kuliko.