Kupitia uzinduzi wa Selcom Lipa Later, tumeleta njia bora na nafuu ya kufanya malipo ya mafuta.

Selcom Pesa imezindua rasmi huduma mpya na ya kwanza nchini Tanzania “Selcom Lipa Later”. Hii ni huduma ya mkopo wa mafuta ya papo hapo isiyo na riba kwa malipo yatakayokamilishwa siku hiyo hiyo kabla ya saa sita usiku. Huduma hii inapatikana ndani ya Selcom Pesa kwenye kipengele cha Lipa.

Ikiwa ni hatua muhimu katika mageuzi ya huduma za kifedha za kidijitali. Uzinduzi huu umefanyika wakati ambapo uhitaji wa huduma za mikopo nafuu na rafiki upo juu. Katika kukidhi gharama za maisha na majukumu ya kila siku yanayohitaji uhakika wa usafiri na ufanisi, mkopo huu ni suluhisho sahihi kwa wateja wetu.

 Katika dhamira yetu ya kuunda suluhisho za kifedha zinazorahisisha maisha, Selcom Lipa Later ni msaada wa kweli na jibu la moja kwa moja kwa wale wanaohitaji mafuta ili kuendelea na kazi na biashara zao bila kukwama.

Selcom Lipa Later imeundwa mahsusi kwa ajili ya makundi yafuatayo;

  1. Madereva wa bodaboda na bajaji wanaohitaji mafuta mara kwa mara ili kuhakikisha kipato cha siku hakiathiriwi na ukosefu wa pesa ya mafuta.

  2.  Wamiliki wa magari wanaotegemea usafiri binafsi kwenye mihangaiko ya kila siku.

  3. Madereva wa usafiri wa mtandaoni, ambao mapato yao yanategemea moja kwa moja uwepo wa mafuta kwenye vyombo vyao vya moto.

  4. Wasimamizi wa huduma za usafirishaji wanaohitaji kudhibiti bajeti na kuhakikisha ufanisi wa magari yao.

Kwa makundi yote haya, Selcom Pesa inatoa urahisi, unafuu na uhakika unaoendana na mahitaji yao halisi bila riba, bila gharama za siri na bila msongamano wa taratibu zisizo na ulazima.

Taarifa muhimu ya huduma hii

Mteja anachagua kituo chochote husika, anaingiza Selcom Lipa Namba au anaskani QR Code, anajaza mafuta, na analipa baadae kabla ya saa 6:00 usiku  bila riba au tozo yoyote ya zaidi. Huu ni uhuru mpya kwa wateja ambao mara nyingi hujikuta wanahitaji kufanya maamuzi ya haraka ili kuendelea na shughuli zao.

Katika kipindi hiki ambacho kila mtu anatafuta namna ya kukabiliana na changamoto za kifedha. Selcom Pesa imekuja na suluhisho linalogusa maisha:

  1. Hakuna kukwama barabarani kwa kukosa mafuta.

  2. Hakuna riba inayokula kipato cha mteja.

  3. Hakuna gharama zilizofichwa.

  4. Hakuna presha ya kulipa papo hapo wakati mahitaji mengine yamepungua kwenye bajeti.

Hii ni nafasi, fursa na hatua muhimu inayowapa Watanzania uhuru wa kujenga mustakabali wao wa kifedha bila kuathiri majukumu yao ya kila siku. Tumejikita kuleta huduma za kidijitali ambazo  zinatoa suluhisho la kweli la changamoto za wananchi.

Tunataka kuona wateja wetu wakifanya shughuli zao kwa amani, uhuru na ufanisi.

Next
Next

The Journey Continues: Selcom Pesa x Mastercard Campaign Extended