Tumezindua rasmi kampeni yetu mpya, “Tumia Bando la Miamala, Kama Bureee.Okoa Gharama!”

Kwa mara ya kwanza Tanzania, Selcom Pesa tumeleta suluhisho jipya lenye unafuu zaidi kwa watumiaji wa huduma za kifedha nchini kupitia uzinduzi wa Mabando ya Miamala. Sasa unaweza kufanya miamala kwa gharama ndogo kupitia huduma hii mpya. Hii ni hatua nyingine muhimu katika dhamira yetu ya kukuhakikishia mteja wetu unapata huduma za kifedha kwa gharama nafuu kabisa. Tulianza na mafanikio makubwa ya kampeni yetu ya "5 kwa Jero," na sasa tunasonga mbele kukupa uhuru zaidi wa kufanya miamala.

Mkuu wetu wa Masoko, Shumbana Walwa, ameleza kuwa Kampeni ya 5 kwa Jero ilituonesha kuwa watanzania wanahitaji suluhisho nafuu na la wazi la kufanya miamala. Tumechukua hatua nyingine mbele kwa kuwaletea Mabando zaidi kwa kila Mtanzania awe na uwezo wa kupanga bajeti ya miamala yake na kuokoa gharama zisizo na lazima. Faida za kutumia bando la Miamala ni;

Lipa Mara Moja, Tumia kadri unavyohitaji: ukishalipia bando lako, hakuna tena ada ya kila muamala ndani ya kikomo chako na kama bando likiisha, unaweza kujiunga tena papo hapo!

Nafuu Zaidi Kuliko Ada za Kawaida: Utapata miamala mingi kwa gharama nafuu sana ukilinganisha na ada za kawaida.

Fuatilia Matumizi Yako kwa Urahisi:Kupitia Selcom Pesa App, unaweza kufuatilia miamala uliyofanya na thamani iliyobaki kwenye bando lako wakati wowote.

Taarifa muhimu za kila bando.

1. 5 Kwa Jero - Bando la Siku

Hii ni kwa ajili ya watumiaji wanaohitaji kufanya miamala michache kwa haraka ndani ya siku. Ukijiunga na bando hili kwa TZS 500 tu, utawezeshwa kufanya miamala 5 BURE ndani ya masaa 24.

2. Wiki Boost - Bando la Wiki

Hili ni bando la kati linalofaa kwa wale wanaofanya miamala mingi ndani ya wiki. Ukijiunga na bando hili kwa TZS 2,500 tu, utapata miamala 35 BURE ndani ya siku 7.

3. Hello Mwezi - Bando la Mwezi

Kwa watumiaji wenye miamala mikubwa na wale wanaofanya Miamala mingi ndani ya mwezi. Ukijiunga kwa TZS 10,500 tu, utawezeshwa kufanya miamala 150 BURE ndani ya siku 30. Anza sasa, jiunge na Mabando ya Mimala kuokoa Fedha zako kwa kufanya miamala bila stress ya makato makubwa.

Ili kujiunga pakua aplikesheni ya Selcom Pesa kutoka Play Store Au App Store na kisha ujisajili mwenyewe ndani ya dakika chache ukitumia NIDA yako tu.

Next
Next

Driving Inclusive Finance through ESG