Wekeza bila gharama na Selcom Pesa kupitia UTT AMIS

Katika hatua muhimu ya kuwezesha Watanzania wengi zaidi kushiriki kwenye uwekezaji, UTT Asset Management and Investor Services (UTT AMIS). Sasa imewezesha uwekezaji kupitia Selcom Pesa bila gharama yoyote kama njia rasmi na salama ya kufanya malipo ya uwekezaji. 

Faida Kuu za Kutumia Selcom Pesa Kuwekeza na UTT AMIS

 Hakuna Makato ukinunua vipande kupitia Selcom Pesa - Tofauti na benki au mtandao wako,Selcom Pesa inakupa uhuru wa  kununua vipande vya UTT bila ada ya miamala.

 Hakuna Kikomo cha Miamala - Kupitia Selcom Pesa, unaweza kuwekeza kiwango chochote bila kikomo.Hakuna masharti ya kiwango cha chini au cha juu, unapata uhuru wa kifedha kulingana na uwezo wako.

 Miamala ya  Haraka - Ukiwekeza kupitia Selcom Pesa, fedha zako zinafika papo hapo kwenye akaunti yako ya UTT AMIS. Hii ni muhimu sana hasa wakati wa fursa au mabadiliko ya haraka kwenye soko.

 Usalama na Uhakika - Taarifa na zako zinalindwa kikamilifu kupitia Selcom Pesa.Ili kuhakikisha uwekezaji wako uko salama kila wakati.

Jinsi ya Kununua Vipande vya UTT AMIS Kupitia Selcom Pesa kiwango chochote bila Makato.

Kununua vipande vya UTT AMIS kupitia Selcom Pesa;

1. Anza kwa kufungua Aplikesheni ya  Selcom Pesa.

2. Chagua  “Lipa Bili”. Baada ya hapo.

3. Nenda kwenye sehemu ya Uwekezaji na uchague “UTT AMIS”. 

4. Weka Namba ya Akaunti yako ya UTT AMIS pamoja na kiasi unachotaka kuwekeza. 

5. Thibitisha taarifa zako na fanya malipo, malipo yako yatathibitishwa papo hapo ni bure kabisa hakuna makato yoyote.

    

Previous
Previous

Fly More, Pay Less: Enjoy Exclusive Emirates & Kenya Airways Offers with Your Selcom Pesa Mastercard.

Next
Next

Weka kikomo cha Matumizi Yako na Selcom Pesa Mastercard.