Weka kikomo cha Matumizi Yako na Selcom Pesa Mastercard.
Ukiwa na Selcom Pesa Mastercard, wewe ndio msimamizi wa matumizi yako. Unaamua kiasi gani utumie yote yapo mikononi mwako.
Kama unataka kupanga bajeti ya matumizi ya kila siku au kuhakikisha familia haitoki nje ya mipango, unaweza kuweka kikomo chako mwenyewe. Hakuna matumizi ya kushangaza, hakuna presha unatumia kadi yako kwa njia inayolingana na maisha yako, kwa uhuru na bila wasiwasi.
Kipi utakosa Ikiwa haujaweka kikomo cha matumizi?
Usipojiwekea kikomo cha matumizi, unaweza ukajikuta hutambui ni kiasi gani umetumia hadi pesa zimeisha. Ni rahisi kuingia kwenye gharama zisizotarajiwa au kuendelea kulipia huduma ambazo hukumbuki hata lini ulihitaji.
Pia, unaweza kuchelewa kugundua kama kadi yako imetumika vibaya. Ukiwa na kikomo, unajilinda mapema, unajitunza, na unakuwa na utulivu wa akili kila unapofanya muamala.